Thursday, 15 May 2014

NEWS>>>Aunt Ezekiel adai talaka.


NYOTA wa sinema za Bongo asiyetabirika
maisha, Aunt Ezekiel amedaiwa

Tuesday, 18 March 2014

HELP: Laptop aina ya DELL inaturn off Display baada ya mda mfupi.

Habari zenu Wadau,

Natumia machine aina ya DELL Vostro, napata tatizo baada ya ku-login to windows inakaa kwa dk1 tu halafu ina-turnoff display, inaendelea kuwa ON. Nimejaribu kuongeza brightness lakini haijawa sawa, pia kwenye ile option ya ya ku-set wakati gani display ijizime iko sawa. Naomba msaada tatizo nini Wakuu?

>>Shilole afungua mgahawa, unaitwa ‘Chuna Buzi Café


Akizungumza kwenye 255 ya XXL, Clouds FM leo,Shilole amesema ameamua kufungua mgahawa kwakuwa ana taaluma ya Hotel Management na pia mama yake alikuwa mama Ntilie.
“Mgahawa wangu ambao natarajia kuufungua hivi karibuni utakuwa naeneo ya Mwananyamala nyumbani ambapo nakaa mimi. Mgahawa utakuwa una vitu vingi za kisasa, kwaiyo chakula kitakuwepo kuanzia mchana mpaka asubuhi yaani. Hii sehemu itaitwa ‘Chuna Buzi Café’ ni jina ambalo nimeamua kuipa kwakuwa ni jina la nyimbo yangu. Kila kitu kipo ni bado tu kufungua.Mimi napenda sana kupika kwasababu mama yangu alikuwa mama Ntilie mkubwa sana na mimi mwanae kwasababu napenda biashara ya vyakula,mimi mwenyewe nimeshasomea Hotel Management kwahiyo najua na najua thamani ya chakula. Kwahiyo mtu ataacha kuvaa lakini atakula chakula, nimefanya kazi ya hoteli, Peacock Hotel, baadaye nikaja nikafanya Florida nikaja kuacha baada ya kupata pesa za biashara,” alisema.

Tuesday, 11 March 2014

RAIS DKT. KIKWETE APOKEA MSAADA WA MAGARI 11 YA KUKABILIANA NA UJANGILI; Meno ya TEMBO 2 yashikwa

Kikwete akitoa hotuba yake kushukuru msaada magari 11 ulioyatolewa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti, Selous na Maswa
Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari 11 kutoka kwa Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (katikati)na kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa.
Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada magari 11 waliyoyatoa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa pili Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro

Monday, 10 March 2014

DALILI ZA MWENZA KUWA NA MPENZI NJE


Leo naomba pia niongelee kuhusu dalili ambazo zinaweza onekana kwa mwenza wako ambazo zinapelekea kujenga fikra kwamba "unasalitiwa" dalili hizo ni kama zifuatazo:-

1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana)
Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae! Anakutumia tu huyo!

2.Sisi ni Marafiki tu!
Kwa amnbao bado hawajaoana Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.Na kwa ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu!

3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu!
Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi wako na ndio maana anakuwa hivyo! Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani!

4.Mabadiliko ya Ratiba za Kazi
Kwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na dharula za kikazi zisizoisha!

5. Kutumia Muda Mwingi katika Computer
Kama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi za ofisini anamalizia!


6. Simu za Siri, Simu kuwa locked!
Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa! Na ya kufanana na hayo!

7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka!
Waswazi wanasema "Wasiwasi ndo Akili" Basi wasiwasi wako huenda ukakupa akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli!

Ukiyaona haya au ya kufanana na haya kaa ukijua kuna kidudumtu kinawala na kitawatenganisha, Ni vyema ukachukua hatua! Pia Jiandae Kudanganywa!

Njia Rahisi ya kupunguza tumbo

  Wengi wa wasomaji wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza mafuta tumboni, wanawake kwa wanaume walituma maswali kwa wingi. Njia iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa ni nani. Alisema kuwa,kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi. Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana. "Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum" anasema. Anasema kuwa kama ntu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani kuwa unaweza kupungua uzito. "Vyakula vya wanga na mafuta ufanya mtu kunenepa, acha au kupunza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa." anasema. Anasema kuwa,tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili. "Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalamu kama glycogem.Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta" Daktari huyo anasema kuwa, mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku.

"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa. "Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni" anasema Daktari. Je Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe? Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Kutokana na hali ya ulaji unaweza kutengeneza manyama uzembe katika kifua, mapaja na maeneo fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea maeneo ya ziada yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa kuwa mafuta. Nishati inayotokana na nafaka ambayop haiwezi kutumika muda huo hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika. Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa wanawake ni asilinia 13 hadi 25. Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika akiba. Kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha bure na kama ukifanya kwa mpangilio na vizuri hutakuwa na shida ya kutengeneza shepu yako. Dk.Martica Heaner,M.A, M.Ed. ambaye hutoa mawaidha ya keep fit ndani ya MSN anasema ni jambo la heri kama mtu atakula kidogo kabla ya kuanza mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya kufanyisha mazoezi. "Lakini kama unaenda mwendo fulani mdogo tu au unatembea kwa dakika 30 huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho kidogo na hasa ikiwa uliweka kitu kiogo saa tatu zilizopita" anasema.

Sunday, 9 March 2014

YOUNG KILLER MSODOKI NAYE AAMUA KUMUONYESHA MPENZI...

 YOUNG KILLER MSODOKI NAYE AAMUA KUMUONYESHA MPENZI...: Young Killer naye ameamua kumusachia mpenzi wake hadharani. kupitia akaunt yake ya Instagram Young Killer Msodoki aliweka picha hizo. Taz...

JINSI YA KUMPATA MSICHANA YEYOTE UNAYEMTAKA KIMAPE...

JINSI YA KUMPATA MSICHANA YEYOTE UNAYEMTAKA KIMAPE...: Kuna wanaume wengi wamekuwa wakikosea kutongoza.Wapo wengine labda amempenda binti fulani lakini anashindwa cha kufanya. Kuna wakati unawe...

>>>Kalenga kwachafuka.....Dereva wa Mwigulu Nchemba ashambuliwa, magari yavunjwa vioo....Diwani wa CCM ajeruhiwa usoni, CHADEMA yadaiwa kuhusika

DEREVA wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Mohamed Kunambi, ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wanaodhaniwakuwa wafuasi wa

Monday, 3 March 2014

Mwigulu Nchemba ataka Dr. Slaa na Freeman Mbowe washitakiwe kwa matukio ya umwagaji damu nchini....Awashangaa polisi kuwaacha wakitanua

MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dk. Willibrod Slaa, wanatakiwa kushitakiwa kwa matukio ya umwagaji damu nchini, linachapisha hivyo gazeti la Uhuru  katika  taarifa ya Suleiman Jongo akiripoti kutoka Iringa

Sunday, 2 March 2014

>>Manchester City wachukua ubingwa wa Capital One

Klabu ya Manchester City jana wamechukua ubingwa Capital One baada ya

NEWS>>> Unapohisi Umechoshwa na Ndoa Yako.

Habari ya mapumziko ya weekend wanajamii,siyo mbaya tukishirikishana hili linaweza kupunguza michepuko ili njia kuu ibaki kuwa salama,turudi katika maada.

Friday, 28 February 2014

NEWS>>>>> Bunge lakanusha tuhuma za paul makonda kuhusika na wizi wa simu bungeni.

Kitengo cha ulinzi na usalama cha Bunge kimetoa taarifa ya kukanusha, tuhuma zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimhusisha Mbunge wa Bunge maalumu la Katiba ndugu Paul Makonda kuhusika na wizi wa simu ya Mjumbe wa Bunge la Katiba. Akitoa taarifa hiyo mbele ya Bunge maalumu la katiba, Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalumu, Mh. Pandu Amiri Kificho alisema;

Marekani kuleta umeme Afrika

Wabunge nchini marekani wameidhinisha mpango wa kuleta umeme kwa zaidi ya watu millioni hamsini katika jangwa la Sahara barani Afrika na hivyo basi kutoa fursa kwa mradi huo wa serikali ya Obama kuanza kutekelezwa.

NEWSS>>Mapenzi ya jinsia moja haramu Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa

NEWS>>>Kalenga: Moja ya hila ya kukusanya vitambulisho vya kupigia kura


Hii ni moja ya mbinu tulizozibaini ambazo zinatumika kukusanya vitambulisho vya kupigia kura. Tangazo hili la vocha za mbolea ya ruzuku lilikuwa limebandikwa kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Igula (just a case study), ni hali ambayo iko maeneo mengi jimboni Kalenga tangu uchaguzi ulipotangazwa. Mgombea Tendega Grace amekuwa akilikemea hilo baada ya wananchi kumpatia malalamiko yao.

Nani atasimama Kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA CHALINZE?

Wanabodi uchaguzi mdogo katika Jimbo la Chalinze umetangazwa na mchakato kwenye vyama vya Siasa unatarajiwa kuanza rasmi.Kwa kuwa Chadema wamepata nguvu kubwa ya ushawishi katika Jimbo hilo,Je Ni nani mnadhani atakuwa mgombea wa chadema?sourse>>jamii forum

Waziri Magufuli akagua mradi wa mabasi yaendayo kasi ( BRT ) jijini Dar.....Barabara ya Kimara hadi Kivukoni kukamilika ndani ya miezi 6 ijayo 2/28/2014 habari za kitaifa

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa  inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama

HATIMAYE Prof. Costa Mahalu, mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri.......

HATIMAYE Prof. Costa Mahalu,
mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri
wa Kanuni zitakazoliongoza Bunge
Maalum la Katiba azungumzia mvutano wa wajumbe wa 'kura iwe wazi ama siri'.Asema, anawaachia wajumbe waamue wenyewe Unadhani hilo ndilo litakuwa suluhisho?.. sourse>>jamii forum

Steve Nyerere ammwagia SIFA Lulu Michael.....Adai ni miongoni mwa wasanii wachache wa kike wasio na skendo chafu kwa sasa

Rais  wa Bongo Movie Unit, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemmwagia sifa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa ni binti mdogo lakini sasa anajitambua tofauti na wasanii wengine wakubwa.

January Makamba na Sugu washiriki kwenye wimbo wa hip hop wa kusisitiza sanaa kutambulika kwenye katiba mpya...

Kilio cha wasanii kuitaka katiba mpya kuitambua sanaa ya Tanzania kama sekta rasmi kimepewa sapoti na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January makamba na mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.

NEWS>>Maneno ya Pnc kuhusu kilichotokea kati yake na Ostaz Juma Namusoma.

Usiku wa kuamkia February 26 uliingia kwenye headline kwenye mitandao ya kijamii na hii ni baada ya kusambaa kwa video na picha zinazomuonyesha Pancras Ndaki Charles au Pnc kupiga magoti mbele ya Ostaz Juma Namusoma kama kumuomba msamaha wa kurudi kwenye kundi.