Kilio cha wasanii
kuitaka katiba mpya kuitambua sanaa ya Tanzania kama sekta rasmi kimepewa
sapoti na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January makamba
na mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Kwa mujibu wa mtandao
wa Bongo5, Makamba na Sugu wameshiriki kwenye wimbo wa hip hop uliowahusisha
rappers 13 wa Tanzania, wimbo wenye lengo la kusisitiza sanaa kutambulika
kwenye katiba mpya. Katika wimbo huo, January Makamba amefanya Intro na Outro
imefanywa na Sugu.
Rappers walioshiriki
kwenye wimbo huo uliopewa jina la ‘Haki’ ni Kala Jeremiah, Quck Rocker, G-Nako,
Nikki wa Pili, Mwana Fa, Danny Msimamo, Profesa Jay, Gosby, Joh Makini, Fid Q
na Kala Pina.
‘Haki’ imetayarishwa
ndani ya Bongo Records na mtayarishaji mkongwe P-Funk Majani.
No comments:
Post a Comment