DEREVA
wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Mohamed Kunambi,
ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wanaodhaniwakuwa wafuasi wa
chama cha
CHADEMA.
Tukio hilo liletokea usiku wa kumkia jana eneo la Ifunda jimbo la Kalenga
wilaya ya Iringa Vijijini mkoa wa Iringa.
Mbali na dereva huyo diwani wa kata ya Ifunda, Eliya Mngwila, naye amejeruhiwa
na watu hao waliposhambulia gari alilopanda.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, wakati
alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mchakato wa kampeni.
Mtenga alisema tukio hilo lilitokea eneo Ifunda ambapo vijana wa CHADEMA
waliokuwa kwenye gari lenye namba za usajili T 156 CDA iliyokuwa na nembo ya
M4C inayotumiwa na chama hicho.
Alisema vijana hao wakiwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapangawalimkuta dereva
huyo pamoja na viongozi wengine wa CCM akiwemo diwani huyo na kuanza
kuwashambulia.
Alisema baada ya tukio hilo waliojeruhiwa walipelekwa Makao Makuu ya Polisi
mkoa wa Iringa abako waliandika maelezo na kupewa kibali cha kwenda hospitali
(PF3).
"Walishambulia magari yetu kwa kuyavunja vioo hivi sasa yako polisi,
tunauhakika waliofanya hivi ni wafuasi wa CHADEMA na hayo ni maelekezo kutoka
kwa viongozi wa juu wa chama hicho," alisema.
Kwa mujibu wa Mtenga, gari la CCM lililoshambuliwa ni lenye namba za usajili T
139 CKS ambalo pia liko Polisi.
Wakati huo huo, CCM imesema CHADEMA imeingiza mkoani humo vijana 120 kwa ajili
ya kufanya vurugu ili kuvuruga mchakato wa uchaguzi huo.
Mtenga, alisema taarifa za uhakika walizonazo, zinasema vijana hao wameingia
mkoani humo juzi na watasambazwa kwenye kata mbalimbali za jimbo hilo.
"Hivi sasa vijana hao wako Iringa mjini wakijiandaa kutekeleza malengo yao
ambapo miongoni mwake ni haya yanayotokea sasa," alisema.
Mtenga alikionya chama hicho na kusema kisithubutu kufanya vurugu hizo kwa
lengo la kumwaga damu kwa wananchi wasio na hatia kwani hakitavumiliwa.
"Kazi ya CCM ni kulinda amani, hivyo hatutakuwa tayari kuona damu ya mkazi
yeyote wa Kalenga inamwagika," alisema.
Akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya kutekwa Paroko wa Kanisa la Orthodox, Parokia
ya Mtakatifu Basil Mkuu , Costantino Mbilinyi, Mtenga alisema ni za uongo.
Akifafanua kuhusu tukio hilo alisema CCM ina watu wenye akili timamu ambao
hawawezi kufanya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Mtenga, siku ya tukio Paroko huyo aliongozana na vijana saba wa
CHADEMA kutoka Arusha kwa ajili ya kufanya vurugu.
Alisema gari alilokuwemo paroko huyo lilikutwa na silaha za jadi yakiwemo
mapanga ambazo zinadhaniwa zilikuwa maalumu kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
"Mwaka 2010 paroko huyo alikuwa mpambe wa Grace Tendega wakati huo akiwa
cha cha Jahazi Asilia ambaye kwa sasa ndiye mgombea ubunge kupitia chama cha
CHADEMA," alisema.
No comments:
Post a Comment