MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam
, imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi
Mawaziri Waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona
wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia
Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi baada ya
kusikiliza maombi yao leo.
Uamuzi huo umetolewa
leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya washtakiwa hao kuwasilisha
maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Upande wa Jamhuri
ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.
Jaji Utamwa alisema
baada ya kusikiliza maombi hayo mahakama inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda
nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na ruhusa hiyo Mramba na Yona siku ya
kusikiliza kesi Aprili 22, mwaka huu wahudhurie mahakamani.
Mbali na Mramba na Yona,
mshtakiwa mwingine ni, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Kesi hiyo imepangwa
kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.
Katika kesi ya msingi,
washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004
jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu
walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa kuwa kwa
kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa
ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS)
Government Business Corporation waliingia mkataba kukagua kiwango cha
uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
TUPE MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment