▼
Thursday, 15 May 2014
NEWS>>>Aunt Ezekiel adai talaka.
NYOTA wa sinema za Bongo asiyetabirika
maisha, Aunt Ezekiel amedaiwa
kudai talaka
kutoka kwa ndugu wa mumewe Sunday
Demonte kufuatia madai kwamba
alikasirishwa na manenomaneno yao kwenye
vyombo vya habari.
Ntaa wa sinema za Bongo asiyetabirika
maisha , Aunt Ezekiel
Kwa mujibu wa chanzo, nyota huyo
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita
jijini Dar baada ya kutua toka Dubai alikodai
alikwenda kwa mume wake .
Ilidaiwa kwamba , mara baada ya kutua
Bongo, Aunt alikutana na shoga yake mmoja
ambaye jina lake halikupatikana mara moja
na kutonywa kuwa kuna gazeti liliandika
habari yake kwamba wakati mumewe
akidaiwa kuwa jela , yeye anaponda raha
Dubai.
“Aunt aliambiwa kuwa wasemaji wakubwa
wa maneno hayo ni ndugu wa mumewe yaani
mashemeji na mawifi zake . Wao wamesema
watawasiliana na mume wake kule aliko , hata
kama ni gerezani, atoe kibali cha ndugu
yeyote wa kiume kuandika talaka na
kukabidhiwa Aunt kwa vile hana uchungu na
matatizo ya mumewe.
AUNT ASHTUKA KWA MANENO YA NDUGU
WA MUME
“Taarifa hizo zilimshtua sana Aunt mpaka
akaonekana kupaniki , akajibu mapigo kwa
kusema ‘ niko tayari kwa talaka , kwanza mimi
mwenyewe ndiyo naomba wanipe talaka .
Kama hao ndugu wanaweza kwenda kwa
Demonte wakapewa kibali cha kunipa talaka
basi mimi nasema naomba wanipe ’ niko
tayari, ” kilisema chanzo hicho kikimkariri
shoga wa Aunt
No comments:
Post a Comment