MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu
Mkuu wake Dk. Willibrod Slaa, wanatakiwa kushitakiwa kwa matukio ya umwagaji
damu nchini, linachapisha hivyo gazeti la Uhuru katika taarifa ya
Suleiman Jongo akiripoti kutoka Iringa
.
Pia, vyombo vya dola vimelaumiwa kwa kukaa
kimya bila kuwachukulia hatua zakisheria licha ya kushiriki katika matukio
yaliyopoteza maisha ya Watanzania.
Hayo yameelezwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, ambapo alisema licha ya viongozi hao kushiriki
kwenye matukio mengi ya vurugu na umwagaji damu, lakini bado wako nje
wakiendelea kutanua.
Alisema iwapo uchunguzi wa kina utafanyika ni
dhahiri Mbowe na Dk. Slaa hawatasalimika na kwamba, ushahidi wa matukio upo
hadharani.
Mwigulu alikuwa akizungumza katika Kijiji cha
Magubike, kata ya Nzihi wilayani Iringa wakati akimnadi mgombea wa CCM Godfrey
Mgimwa, kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga utakaofanyika Machi 16, mwaka
huu.
Alisema Dk. Slaa na Mbowe wanahusika na vifo
vya watu vilivyotokea kwenye vurugu mbalimbali katika mikutano ya hadhara ya
chama hicho.
"Hawa watu
wameshiriki kwenye matukio mengi ya vurugu na yanafahamika, lakini
hawajachukuliwa hatua. Uchunguzi wa kina ufanyike kwani wote hawa wanahusika
moja kwa moja.
"Mikono yao
imejaa damu za watu waliopoteza maisha Morogoro, Singida Arusha na maeneo
mingine ya nchi yetu,"
alisema Mwigulu.
Alisema vurugu zote ambazo zimefanywa na
CHADEMA lengo ni kufanikisha mikakati yao kisiasa, jambo ambalo wananchi wa
Kalenga wanapaswa kuliepuka na kuwa makini nao.
Alisema kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka huu
tayari vifo vya watu zaidi ya nane vimetokea katika mikutano ya Chadema na
kwamba, hali hiyo inapaswa kuonywa vikali na wapenda amani wote.
Pia, alisema viongozi hao wamekuwa wakifadhili
matukio ya vurugu kisha kijitokeza kusaidia familia za waathirika.
Akitoa mfano kwa Mussa Tesha, aliyemwagiwa
tindikali mkoani Tabora wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga na Alphonce
John, aliyetobolewa macho wilayani Kahama, Mwigulu alisema viongozi hao
walihusika na mipango hiyo.
"Historia
inaonyesha kuwa hawa watu wakiwa kwenye mikutano mauaji ni lazima. Tumechoka ni
unyama huu sasa tunataka hatua kali zichukuliwe ili kulinda maisha ya
watanzania,"
alisema.
Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa
Kalenga kukataa viongozi hao kwani, mara zote wamekuwa wakitumia ubabe na
vitisho kutaka kupigiwa kura.
"Ni vizuri
wakamchagua kijana ambaye anaweza kufanya kazi katika mazingira ya amani na
utulivu ili kuzitatua changamoto zilizopo,"
alisema Mwigulu.
Pamoja na hayo, alitumia nafasi hiyo kuweka wazi
Watanzania wanatakiwa makini na vyama vya siasa vyenye lengo la kuvuruga amani
kuwa, CHADEMA hunufaika na vurugu hizo kupitia wafadhili wao
No comments:
Post a Comment