Klabu ya Manchester City jana wamechukua ubingwa Capital One
baada ya
kuifunga Sunderland bao 3 kwa 1.
Sunderland ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na
mshambuliaji wake Fabio Borini katika dakika ya kumi ya mchezo,mpaka mapumziko
Sunderland ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Manchester City ilidhamiria kupata ushindi huku
wakizidisha mashambulizi langoni mwa Sunderland.
Juhudi zao zilianza kuzaa matunda, ambapo katika dakika ya 55
Yaya Toure alifyatua kombora lililotinga wavuni moja kwa moja na kuisawazishia
timu yake. Dakika moja baadaye dakika ya 56, Samir Nasri alifunga bao la pili
kwa mkwaju mkali na kumwaacha mlinda mlango wa Sunderland, Mannone akishangaa
kinachotokea.
Jesus Navas ambaye alichukua nafasi ya Kun Aguero, alikomelea
msumari wa moto katika jeneza la Sunderland baada ya kupachika goli la tatu
katika dakika ya 90.Hadi mwisho wa mchezo vijana wa Pellegrini waliibuka
mashujaa na kutawazwa ubingwa wa kombe hilo la Capital One, likiwa kombe lake
la kwanza la ubingwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment