KOMPYUTA zinazotumia
windows XP
hazitoweza kupokea taarifa muhimu na kuongezeka mashambulizi ya
virusi vya spyware vinavyoharibu taarifa binafsi na takwimu za kibiashara baada
ya mwezi mmoja. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Microsoft
kwa kanda za Afrika Mashariki, Magharibi, Rotimi Olimide.
Alisema kuwa utafiti
mpya wa Microsoft umeonyesha kuwa Window XP hushambuliwa kirahisi na virusi
mara tano zaidi huku usalama wake ukiwa mdogo kiasi cha kuruhusu wizi wa
mtandao.
Alisema ni vyema ndani
ya mwezi mmoja, watumiaji wa window hiyo wakabadilika na kuhamia Window 8
ambayo ina uwezo mkubwa wa kuhimili mshambulizi ya virusi.
“Mfumo uliotengenezwa
kwenye Window XP ni wa kizamani na uendeshaji wake sio iliyoundwa kujilinda
dhidi ya virusi.
“Baada ya mwezi mmoja
si kuwa huduma ya Window XP haitafanya kazi, unaweza kuendelea nayo lakini
usalama na utendaji wake hautakuwa mzuri ,” alisema.
Alisema mfumo wa
uendeshaji wa Windows 8 na Office 365 unatoa ulinzi wa uhakika na ufanisi.
Mkurungezi wa Teknolojia na Uendeshaji, Chege Thumbi alisema ni vyema hasa
taasisi za kifedha kuacha kutumia windows XP mara moja ili kuwa katika usalama
na urahisi wa kufanya biashara.
No comments:
Post a Comment