Thursday, 15 May 2014

Tuesday, 18 March 2014

HELP: Laptop aina ya DELL inaturn off Display baada ya mda mfupi.

Habari zenu Wadau,

Natumia machine aina ya DELL Vostro, napata tatizo baada ya ku-login to windows inakaa kwa dk1 tu halafu ina-turnoff display, inaendelea kuwa ON. Nimejaribu kuongeza brightness lakini haijawa sawa, pia kwenye ile option ya ya ku-set wakati gani display ijizime iko sawa. Naomba msaada tatizo nini Wakuu?

>>Shilole afungua mgahawa, unaitwa ‘Chuna Buzi Café


Akizungumza kwenye 255 ya XXL, Clouds FM leo,Shilole amesema ameamua kufungua mgahawa kwakuwa ana taaluma ya Hotel Management na pia mama yake alikuwa mama Ntilie.
“Mgahawa wangu ambao natarajia kuufungua hivi karibuni utakuwa naeneo ya Mwananyamala nyumbani ambapo nakaa mimi. Mgahawa utakuwa una vitu vingi za kisasa, kwaiyo chakula kitakuwepo kuanzia mchana mpaka asubuhi yaani. Hii sehemu itaitwa ‘Chuna Buzi Café’ ni jina ambalo nimeamua kuipa kwakuwa ni jina la nyimbo yangu. Kila kitu kipo ni bado tu kufungua.Mimi napenda sana kupika kwasababu mama yangu alikuwa mama Ntilie mkubwa sana na mimi mwanae kwasababu napenda biashara ya vyakula,mimi mwenyewe nimeshasomea Hotel Management kwahiyo najua na najua thamani ya chakula. Kwahiyo mtu ataacha kuvaa lakini atakula chakula, nimefanya kazi ya hoteli, Peacock Hotel, baadaye nikaja nikafanya Florida nikaja kuacha baada ya kupata pesa za biashara,” alisema.

Tuesday, 11 March 2014

RAIS DKT. KIKWETE APOKEA MSAADA WA MAGARI 11 YA KUKABILIANA NA UJANGILI; Meno ya TEMBO 2 yashikwa

Kikwete akitoa hotuba yake kushukuru msaada magari 11 ulioyatolewa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti, Selous na Maswa
Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari 11 kutoka kwa Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (katikati)na kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa.
Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada magari 11 waliyoyatoa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa pili Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro