Kampuni ya Strabag International GmbH
inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa
jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa
sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama
mkataba wao unavyoelekeza.
mkataba wao unavyoelekeza.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo
wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara
kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus
Rapid Transit – BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha
kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.
Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo
Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli
kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea
kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika
hatua hii iliyobaki.
Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na
vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika
katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara
hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu
ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime
na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya
kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia
kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
Waziri Magufuli akizungumza wakati wa
kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo
kwa muda na viwango vilivyokusudiwa. “Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi
ni lazima sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha
anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo
hilo la barabara kinyume na sheria.
Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa
kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City
Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda
kirefu. “Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza
kutoa visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe.
Magufuli.
Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli
amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo
upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa
zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika
njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa
eneo kati ya Ubungo na Kiamara.
Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS
Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa
haraka utajengwa katika awamu sita.
Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu
unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara –
Kivukoni, Magomeni – Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha
kamilisha asilimia 55 ya mradi wote.
****************
****************
Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuli Kituo cha BRT kivukoni jijini
Dar es salaam leo akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Waziri wa Ujenz Dkt.
John Pombe Magufuli (aliyekaa kulia) akiwa na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe (katikati) pamoja na Mtendaji Mkuu wa
TANROADS Eng. Patrick Mfugale (aliyesimama) wakisafiri kwa basi kukagua
utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es
Salaam
Mkurugenzi
Mkuu
wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka
kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa Mradi wa Mabasi
yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti)
akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam
.jpg)
Msimamizi wa Mradi wa
Mabasi
yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti)
akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam .sourse>>mpekuzi
No comments:
Post a Comment